Activities in & around

Walk to the top of Mt. Rungwe

SAFARI YA KUPANDA MLIMA WA TATU KWA UREFU TANZANIA (MLIMA RUNGWE)
ofisi ya mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Rungwe kupitia kitengo cha utalii na mali asili wameandaa safari ya siku moja ya kupanda mlima Rungwe jumamosi ya tarehe 27/08/2016.

Gharama ni Tsh 7000/= Kwa washiriki mliopo maeneo jirani na Rungwe na mliopo mbeya ni Tsh 15000/= ikihusisha nauli na kiingilio cha hifadhi. Washiriki kama mkuu wa wilaya na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya, MH mwenyekiti wa halmashauri, WAH madiwani, Mkurugenzi mtendaji, kamati ya utalii ya wilaya, wakala wa misitu (TFS), wild life conservation society (WCS) african wild life foundation (AWF), na wadau mbalimbali watakuwepo, nyote mnakaribishwa. unakosaje kwa mfano ?? Hii si ya kusimuliwa…… Twende tukapande mita 2981 tukianzia Unyamwanga na kuteremkia syukula

Kwa mliopo Rungwe na maeneo jirani piga simu no afisa utalii 0758104873 na afisa maliasili na utalii (W)  0763641150.